Responsive Ads Here

Sunday 8 April 2018

Kutana na kifaa chenye uwezo wa kusikia mawazo yako .

Teknolojia inaonekana kukua siku hadi siku na hii ina dhihirika wazi kwa kuwa wanasayansi wanaendelea kugundua vitu tofauti tofauti.Leo nimewaletea hii ya kifaa kipya chenye uwezo wa kusikia mawazo yako.

Kifaa hicho kimetengenezwa na wanasayansi kutoka katika chuo cha MIT huko nchini Marekani,na inasemekana kifaa hicho kwa sasa kina uwezo maalum wa kusikia mawazo yako na kuyapeleka moja kwa moja kwenye kompyuta.Kwa maana nyingine ni kwamba, kifaa hicho kinasaidia mtu kufanya mambo mbaklimbali kwenye kompyuta au vifaa mbali mbali vya kielektroniki kwa kutumia au kusikiliza mawazo yako.

                                         
                                                               
Kifaa hichi kinafanya kazi kwa kupima signal maalumu zinazo husika na mawazo ya ubongo kwenye uso wako zinazoitwa Neuromuscular signal sasa signal hizo hutaffiri kwa kutumia mfumo wa Al au artificial intelligence ambao hubadilisha signal hizo kwenda kwenye mfumo wa program ambayo husaidia vitu vya kielectronic kwenda kufanya kazi,yaani kama vile rimoti ya TV yako inavyo fanya kazi,ila mawazo yako ndiyo mkono wako.

Kwasasa kifaa hicho kina uwezo mdogo kama wa kama wa kusema saa pale utakapo waza ni muda gani,kutumika kuchagua program mbalimbali kwenye TV amoja na mambo mengine madogo madogo.Vile vile kwa mwonekano kifaa hicho bado ni kikubwa sana labda miaka ya karibuni kifaa hicho kita boreshwa na kuwa kidogo.

No comments:

Post a Comment