Responsive Ads Here

Monday 2 April 2018

Ilivyo kuwa siku ya wajinga kwa upande wa teknolojia

Siku ya wajinga ni siku ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 mwezi wa 4.Kwa mwaka huu siku hii ilikuwa ya tofauti sana kwa wapenzi wa teknolojia kwani vimetokea vitu vingi sana ambavyo vimekuwa gumzo maka mda huu.

23ANDME + LEXUS          

Eti kwa kutumia mate yako unaweza kupata gari la lexus lenye kuendana na wewe pamoja na kulingana na harufu yako na kuwasha gari lako hauhitaji funguo bali ulimi ndiyo unatumika kuwashia gari.Duh




AMAZON PUBLISHING


Siku ya jana yenyewe ilizindua AMAZON PUBLISHING. Hii ni huduma ambayo unaweza kumwita mwandishi wa kitabu unaye mpenda popote pale alio na kuja hadi kwenye mlango wako yani hata kama yuo wai na muda wowote anakuja hapo hapo.




ROKU

Kampuni ya ROKU yenyewe imekuja na Teknolojia ya kukuwezesha kutumia TV yakoa kwa namna ya kipekee.ROKU ina kuletea streaming soksi,soksi hizi zitakusaidia kutoshika rimoti yako na badala yake utakuwa na uwezo wa kutumia rimoti yako kwa kutumia soksi.



SODASTREAM

Hii ni aina mpya ya maji ya kisasa yenye uwezo wa kufanya mwili wako uwe una jisikia vizuri na kikubwa zaidi maji haya yanakufanya usizeeke


T-MOBILE

Teknolojia imekua sana kiasi kwamba kuna simu mpya ya kisasa kabisa ambayo ni SIMU YA KIATU.Ambayo inakupa uwezo wa kufanya mambo mengi sana kama inavyoonekana kwenye video hapo chini.







 

No comments:

Post a Comment